Kongamano la kupinga mauaji ya albino Geita

Kufuatia kukithiri kwa vitendo vya kikatili vya mauaji ya ndugu zetu walemavu wa ngozi, wadau wa haki za bindamu mkoani Geita wamepanga kufanya kongamano kubwa kulaani vitendo hivyo mnamo tarehe 6, april 2015. Mmoja kati ya waratibu wa kongamano hilo ambaye pia ni mkurugenzi wa Acts Counsillor Tanzania amesema, "Ni zamu ya wakazi wa Geita kuonesha hisia za kuguswa na kadhia hii.Ni aibu kwa taifa letu linalojinasibu kuwa kisiwa cha amani kukiuka haki za binadamu waziwazi". Naye mhamasishaji wa mabadiliko kwa vijana (YOUTH FOR CHAMGE)maarufu kwa jina la Boniphace amesema kongamano hilo litashirikisha viongozi wa dini, waumini,wanasiasa,wazee kwa vijana pamoja na viongozi wa serikali. Kongamano hilo limepangwa kufanyika katika ukumbi wa Gold Belt Geita, karibu na stendi mpya ya Geita. UKWELI MTUPU BLOSPOT INAWATAKIA KILA LA KHERI.