Kichaa wa mapenzi `1

Kichaa wa mapenzi `1

 Majira ya saa nane mchana kukiwa na hali ya hewa ya kamvuamvua kiidogo katika barabara ya Mandela rodi gari la abiria lililokuwa likitokea Ubungo kuelekea Gongolamboto liliacha njia na kwenda kuingia mtaroni na kusababisha kupinduka. Watu waliokuwa jirani na ajari hiyo walikimbia kwenda kuokoa majeruhi pia wapo ambao walikuwa wakiwahi katika gari hiyo kwa nia ya kuiba, Japo ajari haikuwa kubwa sana lakini wapo waliovunjika na wengine kupelekea kupoteza fahamu lakini kwa kuwa eneo la Buguruni halipo mbali sana na kituo kikubwa cha polisi haikuchukua mda askari walifika na kuendeleza utaratibu wao, Baadhi ya wahanga wa ajali walikimbizwa hospitali ya Amana lakini kuna mmoja ambae hali yake haikuwa nzuri alipofika amana jopo la madaktari wa hospitalini hapo walisema akimbizwe katika hospitali ya taifa Muhimbili, Alipofikishwa hapo alipokelewa na wahudumu wa hapo na kupelekwa moja kwa moja chumba cha wagonjwa mahututi. ***** Mzozo mkubwa unaibuka kati ya wapenzi wawili kwa sababu ya wivu wa kimapenzi unaopelekea mmoja wao kuinua kitu kizito na kumtwika mwenzie sehem ya kichwa hadi kumpelekea kumuendesha chini mpenzi wake, Baada ya kuona hivyo hakutaka kupoteza mda kabisa alikimbia na kumuacha mwenzake hajitambui, Zuhura binti wa kazi wa nyumba ile wakati akiwa katika harakati zake za kuweka sawa mazingira ya nyumba aliisikia simu ya bosi wake ikiita kwa muda mrefu bila kupokelewa mara kwanza hakutilia mkazo sana alijua labda bosi wake ndivyo alivyoamua lakini baadae wazo likamjia aende chumbani kwa bosi wake huenda akawa amelala, Aliposogelea eneo la mlango wa chumba cha dada yake alishangaa kuuona mlango upo wazi kabisa alipoangaza macho alimuona bosi wake akiwa chini ajielewi kabisa. Zuhura alizidi kushangaa na hali aliomkuta nae bosi wake aliinamana kumtingisha huku akilitaja jina la Mungu wa viumbe wote lakini hakukuwa na dalili ya kustuka kwa bosi huyo. Mwisho aliamua kupiga simu polisi mda mchache walifika na kuchukua maelezo yake na baada ya hapo alichukuliwa mgonjwa na kukimbizwa hospitali ya taifa. Polisi walimchukua Zuhura kwa ajiri ya maojiano zaidi, "Binti huyu dada we upoje nae?" Aliuliza askari mmoja mweusi mwembaba "Ni bosi wangu" "Una mda gani tangu uanze kazi kwake?" "Miezi miwili tu" "Unaweza kutueleza nini kilichopelekea bosi wako kuwa katika hali ile? "Hapana mimi sijui, mimi sijui kabisa kaka afande!" "Usinifiche kumbuka ukileta masihara unaweza ukadondokea vyombo vya dola" Yule askari aliongea huku akimkazia macho Zuhura! "Kweli kaka afande mie sijui" Askari aliinama chini huku akiandika andika badae alimuita askari mwenzie na kumuamrisha ampeleke mahabusu Zuhura, Maskini mdada wa watu alilia huku akilalamika sijafanya kitu!! sijafanya kitu!! lakini kama tunavyojua kelele za chura azimzuii tembo kunywa maji Zuhura aliingizwa mahabusu kisha geti lilifungwa kwa mtindo wa kubamizwa kwa nguvu...... Itaendeleaaa