TISHIO LA UGAIDI NCHINI TANZANIA.

TISHIO LA UGAIDI NCHINI TANZANIA.

                                              TISHIO LA UGAIDI NCHINI TANZANIA

        Ni siku kadhaa zimepita tangu ndugu zetu wakenya kupata msiba mkubwa  uliosababishwa na shambulio la kigaidi.Shambulio hilo lililofanya na kundi la kigaidi la Al shabab lilikatiza maisha ya takribani wanafunzi 145 katika chuo kikuu cha GARISA nchini Kenya.

        Na baada ya siku chache tangazo lingine lilitoka kwa kiongozi wa kundi la IS akimpongeza kiongozi wa kundi la Al shabab kwa kutekeleza shambulizi la kinyama kabisa.Kando ya pongezi hizo pia kiongozi huyo aliliagiza kundi la Al shabab kufanya mashambulizi katika nchi za Ethiopia,Uganda,Tanzania na Burundi.Katika taarifa iliyotolewa na kituo cha kimataifa cha Al Jazeera,na kutafsiriwa kwa lugha ya kifaransa na kiswahili,kiongozi huyo ameagiza kulengwa kwa miji mikubwa ya Tanzania ya Dar es salaam na Mwanza.

    Serikali yetu haipaswi kupuuza vitisho hivi kwani suala la ugaidi si jambo la kupuuza hata kidogo.Serikali ya Tanzania inapaswa kutafakari ni hatua gani kuchukua ili kulinda raia wake.Kwa kutumia vyombo vyote vya ulinzi na usalama ,serikali inapaswa kuwahakikishia raia wake usalama wa wakati wote.

       Kwingineko viashiria vya ugaidi vimeanza kujitokeza hapa nchini hasa tukiangalia matukio yaliyojitokeza mwaka 2014 katika jiji la Arusha na kule Zanzibar.Matukio yale yalikuwa yanaikumbusha serikali kwamba chochote kinaweza kutokea katika ardhi ya nchi hii.

      Tunaomba mungu atuepushie balaa hili .

by frank lungwa

[email protected]

[email protected]

+255785192891