Tanzania Youth Ability

TANZANIA YOUTH ABILITY

(T.Y.A)

 

MWONGOZO WA KIKUNDI CHA T.Y.A

Kikundi hiki kimeundwa kwa malengo ya kujenga na kudumisha umoja uliopo miongoni mwa vijana sambamba na kutafuta fursa mbalimbali zinazo mhusu kijana ili iwe kama njia ya kumuinua kiuchumi. Pamoja na kutoa misaada kwa jamii ya watu tegemezi kama msingi wa kujenga jamii ya matumaini. Pia kwa namna nyingine kutangaza sanaa na utalii wa TANZANIA ndani na nje ya nchi kwa kuanzisha vikundi mbalimbali vya sana apamoja na dhihara za kirafiki katika vituo mbalimbali vya kitali inchini.

 

MALENGO YA T.Y.A

  1. Kujenga na mshikamano kwa vijana pamoja na kuandaa vijana wenye moyo wa uzalendo na wautayari kutumikia na kujivunia utaifa wao.
  2. Kusaidiana na kushirikiana katika matatizo na changamoto mbalimbali zinazo mkabili kijana katika mazingira yanayomzunguka pia kujenga familia ya vijana iliyo ya mfano wa kuigwa na vijana wengine.
  3. Kusajili umoja huu ili utambulike na serikali, jamii na ulimwengu kwa ujumla na kuanzisha matawi yake sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi ya TANZANIA.
  4. Kuanzisha  miradi mbalimbali na kutafuta fursa katika jamii inayotuzunguka ili kuweza kujiingizia kipato kama kundi sambamba na kumuinua kijana kiuchumi.
  5. Kutembelea na kutoamisaada kwa jamii ya watu tegemezi na kujenga jamii ya matumaini.
  6. Kuanzisha na kusimamia vikundi mbalimbali vya sanaa ambavyo vitatoa fursa kwa vijana kutumia vipaji vyao kama sehemu ya kujiingizia kipato.
  7. Kutangaza sanaa yetu sambamba na utalii ndani na nje ya TANZANIA.

 

N.B: kati ya malengo tajwa hapo juu yapo baadhi yameafikiwa sambamba na uanzilishi wa umoja wa T.Y.A kwa baadhi ni kama uanzilishi wa kikundi cha uigizaji cha ENTERTAIMENT-ARTIST-GROUP pamoja na kikundi cha uimbaji cha T.STAR-VOICEhttp://facebook.com/entertaiment-artist-group