Hizi ni sababu za Memphis Depay wa Man United kutotumia jina la baba yake katika jezi.

Hizi ni sababu za Memphis Depay wa Man United kutotumia jina la baba yake katika jezi.

 

Winga mpya wa klabu ya Manchester United Memphis Depay ameingia kwenye headlines, kama ambavyo huwa ni kawaida kwa mastaa kuingia katika headlines za vyombo vya habari kutokana na maisha yao na uwezo wao uwanjani, safari hii winga huyo wa Kiholanzi ameingia kwenye headlines baada ya kugoma kutumia jina la baba yake.

memphis-depay

Memphis Depay mwenye umri wa miaka 21 amegoma kutumia jina la baba yake katika jezi yake anayovaa, siku zote imezoeleka kuona wachezaji wengi hupenda kutumia majina ya baba zao katika jezi au hata maofisini, ila hii ni tofauti kidogo kwa winga huyo, kwani amegoma kutumia jina la baba yake, kwa sababu alimuacha toka akiwa na umri wa miaka minne.

Memphis Depay

Baba yake kaomba msamaha kwa kosa hilo, Memphis bado hajajibu chochote ila baba yake alihojiwa na the sun na kumuomba mwanaye huyo wasahau mgawanyiko uliyokuwepo kati yake kwa miaka 17 iliyopita.