Utangulizi Misingi ya katiba

Kwa kuwa sisi wananchi wa jamhuri ya mungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru,haki,udugu na amani.

Na kwa kuwa misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye demokrasia ambayo serikali yake husimamiwa na bunge lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowakilisha wananchi na pia yenye mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote, na hivyo kuhakikisha kwambahaki zote za binadamu zinadumishwa na kulindwa, na wajibu wakila mtu unatekelezwa kwa uaminifu:

KWA HIYO,BASI,KATIBA HII IMETUNGWA NA BUNGE MAALUM LA JAMHURI YA MUUNGANO TANZANIA, kwa niaba ya Wananchi, kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, napia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa na serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia na ujamaa.