TWITTER YAMPONZA GUARDIOLA

TWITTER YAMPONZA GUARDIOLA TWITTER YAMPONZA GUARDIOLA...... Mara nyingi wachezaji huwa na ndoto za kupenda kucheza timu kubwa ama kujiunga na vilabu kama Barcelona,Real Madrid,Chelsea,Man U na Juventus lakini mchezaji mmoja ametimuliwa muda mfupi tu baada ya kujiunga na klabu ya Barcelona ya Nchini Hispania kutokana na mtandao wa kijamii.. Mshambuliaji Sergi Guardiola alikuwa ametia saini mkataba wa kujiunga na timu ya akiba ya Barcelona Lakini saa chache baadaye alijikuta akitimuliwa mbio Mara baada ya maafisa wa klabu hiyo walipojulishwa kuhusu “jumbe za kuudhi kwenye Twitter” ambazo aliziandika miaka miwili iliyopita kuhusu Barca na jimbo la Catalona. Guardiola mwenye umri wa miaka 24, aijiunga na Barcelona B Jumatatu, lakini kwa mujibu wa gazeti la michezo la Uhispania la Marca, mkataba wake ulibatilishwa pindi klabu ilipogundua alikuwa ameandika jumbe za kuunga mkono mahasimu wakuu wa Barcelona Real Madrid kwenye Twitter. Aidha, alikuwa ametumia lugha ya kuudhi dhidi ya wakazi wa Catalona, jimbo linalopigania kujitenga kutoka kwa Uhispania. Guardiola alianza msimu huu akichezea klabu ya Alcorcon ya jiji la Madrid ambayo imekuwa ikicheza ligi ya daraja la pili Uhispania.