JE WAJUA YA KWAMBA MATOKEO YA FORM FOUR KUTANGAZWA JUMAPILI?

JE WAJUA YA KWAMBA MATOKEO YA FORM FOUR KUTANGAZWA JUMAPILI?

Watanzania wenzangu tumezowea kusikia mambo mengi kujitokeza baada ya matokeo kutoka, hasa swala la wanafunzi wengi kuwa na uamuzi mgumu (kujinyonga au kujiua) baada ya matokeo ya mtihani wake kutoka vibaya. Mimi kama Mtanzania mwenzenu ninapenda kutoa tahadhari kwa wale wote ambao huwa wanakua na uamuzi wa namna hii, tafadhali kama unajua huwezi kujizuwia kufanya mambo haya omba ushauri kwa watu au ndugu zako nao watakusaidia. Maisha sio kusoma tu bali kuna mambo mengi duniani ya kufanya ambayo yanaweza kukufanya kufikia malengo yako, japo elimu ina sehemu yake kukufanya ufikie malengo hayo.

Kwa wale ambao ni wacha Mungu unaweza ukamwoomba Mungu wako kwanza kabla ya kuyaangalia matokeo yako, kwa sababu hayo maamuzi mengine ya kuanza kufikilia kufanya mabaya huwa yanakuja pale tu unapoona matokeo hayo. ninasema haya kwa sababu Mungu hana mpango wa kuwapoteza watu wake kwa namna hii, bali ni mpango wa kishetani. 

Nawatakia kila la heli